| |
Kabla ya harusi
- Kama utafanya engagement party basi panga siku kabisa
- Utafanya kitchen party au bridal shower? Anza maandalizi
- Siku yako ya Send off
- Unafikiria kufanya nini kwenye fungate? Fikiria maandalizi
Harusi yako
ZINGATIA
Kwa kila malipo unayofanya usisahau kuandikishana au
kuchukua stakabadhi (receipt)
- Ni vema kuwa na jalada ambapo utahifadhi habari zako zote
kuhusiana na harusi yako
- Fikiria unataka harusi ya aina gani, ndogo – watu wa
karibu tu, kubwa na ya kifahari, ya kati kati, ukumbi wa nje?
Ndani?
- Kuna watu wanatoka mbali watakaohitaji malazi? Fanya mipango
sasa
- Ndugu jamaa na marafiki wanaweza kuwahifadhi?
- Fanya booking na hoteli au Nyumba za wageni
- Amua unataka kutumia kiasi gani cha pesa na wapi pa kukipata – Unaweza
kupata msaada hapa
- Chagua siku yako ya harusi, vigezo vyaweza kuwa muda wa watu
wenu wa karibu au upatikanaji wa ukumbi au kanisa fulani, angalia
kama ni siku ya sikukuu
- Umeshaamua rangi ya harusi yako?
- Umeshachagua wasimamizi wako? Wataarifu na kuwaeleza nini
unategemea toka kwao
- Je kuna mila au tamaduni zozote ambazo inabidi kuzitilia maanani?
Fanya utafiti. Baadhi ya makabila hufanya hivi
- Andaa ratiba ya harusi
- Usiku wa harusi, fanya booking ya hotel
- Paki kabisa vitu kwaajili ya usiku wa harusi, kama kuna vinavyokosekana
fanya mipango ya kununua
- Je utasafiri kwaajili ya fungato? Fanya booking sasa
Hakikisha una passport, viza, chanjo (kadi ya njano)
|
|