| |
MAVAZI NA UREMBO
Gauni
- Bi Harusi, anza kufikiria nguo yako ya harusi, unataka gauni
la aina gani, agalia mifano hapa. Uliza maswali muafaka
- Nguo ya bi harusi, umeshaamua ni aina gani? Au umeiona haswa
unayoitaka?
- Kama nguo yako ni ya kununua, nenda kaijaribu, kama ni ya
kushona fikiria au pata ushauri juu ya mafundi wa nguo za harusi,
unaweza kuanza na hawa
- Gauni la harusi vipi? Kama umepima na umepata unachotaka lipia
na chukua, kama ni la kushonesha anza kushona kwa fundi uliyemchagua,
mtajie siku ya harusi ambayo ni mwezi mmoja kabla ya harusi
- Kama gauni ni la kukodisha hakikisha umelipeleka kusafishwa
dry cleaner
- Anza kutafuta nguo za wasimamizi wako, watanunua au kushona?
Shela and weaving au rasta
- Mara nyingine gauni haliji na shela unayoitaka, anza kutafuta...angalia
maduka ya nguo za harusi
- Unafikiria kushonea weaving au kusuka rasta, aina gani na
mtindo gani? Angalia mifano hapa
Mapambo mengine
- Hereni, Chain, bangili, viatu, gloves, pochi, vibanio
SALUNI
Nywele na vipodozi
- Nywele, unataka ziwe vipi? Kama utasuka rasta panga siku kabisa
na book msusi
- Chagua saluni utakayopambiwa, ni vema kuchagua saluni inayotoa
kuhuma zote unazohitaji
- Fanya majaribio ya utakavyobana nywele
- Unaweza kutaka kukata nywele pia, style gani?
Ngozi na kucha
- Fanya miadi ya kutengeneza kucha (pedicure, manicure) na kutengeneza
ngozi (facial, waxing)
- Ni vema kufanya shughuli hizi mapema kabla ya siku ya harusi
BWANA HARUSI
Suti ya bwana harusi
- Mkumbushe bwana harusi kufuatilia nguo yake na m(wa)simamizi
wake
Mapambo ya bwana harusi
KANISANI/MSIKITINI/KAMISHNA
- Andikisha harusi yenu walau mwezi mmoja kabla ya siku
- Kuna semina mbalimbali makanisani na misikitini kwa maharusi
watarajiwa, chunguza ni lini na fanya mpango kuhudhuria
MAUA NA MAPAMBO
- Wapambaji – angalia baadhi ya mapambo
- Chagua uliyeridhishwa naye na kukubaliana aina ya mapambo
na maua
- Usisahau maua ya bibi harusi kama utapenda
Ingia naye makubaliano na lipia gharama za awali
|
|