| |
USAFIRI
- Tengeneza ratiba ya usafiri na ni magari mangapi na ya aina
gani yanatakiwa
- Tafuta usafiri, kama ni wa kukodi ni vyema kuyaona magari.
Wanaotoa huduma hii
- Fanya malipo ya awali na kukubaliana mpango wa safari
ZAWADI
- Unataka zawadi gani, chagua zawadi zako ili usipate seti kumi
za sahani na vikombe, ziorodheshe hapa
MENGINEYO
- Kama kuna maonesho yoyote maalumu yaandae na kuyaweka katika
ratiba
- Usisahau kitabu cha wegeni kama utataka
- Jiandae mapema kwa fungate, nunua vitu utakavyohitaji mapema
kabla ya harusi, vipaki kabisa
Kwa kila malipo unayofanya usisahau kuandikishana au
kuchukua stakabadhi (receipt)
Mara mahali, saa na utaratibu utakapokua kamili, wasiliana
na watoa huduma wako wote ili wajue jinsi ya kutekeleza kazi
zao na kufanikisha shughuli yako
Gawa majukumu:
Kukaribisha wageni
Kupokea zawadi
Kutambulisha ndugu
Kumalizia malipo kwa watoa huduma wako – mtu huyu awe unayemuamini,
si ajabu mtakua naye katika safari yote ya kuandaa shughuli yako
Wedding theme/Dhana za harusi
Unajua kwamba unaweza kuipa harusi yako dhana Fulani? Hebu angalia
mifano:
Classic white wedding
Traditional wedding
Beach wedding
Cocktail wedding
Barbecue
|
|